Kiongozi huyo wa UNRWA aidha ameeleza kuwa, "Wakazi wengi zaidi sasa huko Gaza wanalazimika kuyahama makazi yao na kuhamia maeneo yasiyojulikana."
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Quds likinukuu kanali ya Televisheni ya Al Jazeera, Lazzarini ameongeza kuwa: "Katika muda wa siku nne pekee zilizopita, majengo 10 ya shirika hilo la UNRWA huko Gaza yalilengwa na mashambulizi ya utawala wa Israel."
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) hapo awali alifichua katika taarifa yake kwamba takriban watu 2,000 huko Gaza walilengwa na kuuawa shahidi walipokuwa wakitafuta msaada wa chakula, na wengi wa wahanga ni wale waliokuwa wamekusanyika karibu na vituo vinavyojulikana kama "Taasisi ya Kibinadamu ya Gaza" chini ya usimamizi wa Marekani na Israel.
Lazzarini alionya kwamba kushughulikia mzozo wa njaa huko Gaza kunawezekana tu ikiwa kuna ufikiaji endelevu, ulioenea na salama kwa wale wanaohitaji.
Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umesema una wasi wasi mkubwa juu ya hali mbaya sana ya maisha katika Ukanda wa Ghaza sambamba na kushadidi mashambulizi ya mabomu na makombora yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo lililowekewa mzingiro.
Tangu mwishoni mwa Mei, wakati shirika linaloendeshwa na Marekani la GHF lilipoanza kusambaza misaada, karibu watu 2,500 wameuawa kwenye au karibu na vituo vya utoaji misaada hiyo.
Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu utawala wa kizayuni wa Israel ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza mnamo Oktoba 2023 imeshapindukia 64,800.
342/
Your Comment